KILICHOWASHANGAZA MASHABIKI BAADA YA MOURINHO KUZUNGUMZIA PENATI ILIYOPIGWA NA DROGBA
Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amewashangaza waandishi
wahabari baada ya kusema hakufurahishwa na kitendo cha kiungo
mshambuliaji Eden Hazard kumuachia mshambuliaji Didier Drogba kupiga
penati ya kwanza iliyopatikana wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa
barani Ulaya uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko jijini London
nchini Uingereza.
Mourinho, amesema jukumu la kupiga penati katika kikosi chake lipo
mikononi mwa Eden Hazard lakini cha kushangaza alimuona kiungo huyo
kutoka nchini Ubelgiji akimpa ruhusa Drogba kutimiza jukumu ambalo
halikumuhusu.
Mourinho, amesema hakufurahishwa na kitendo hicho na amewataka
waandishi wa habari kutambua wazi kwamba chaguo lake katika jukumu la
kupiga penati inapojitokeza katika michezo ya The Blues ni Hazard na si
kwa mchezaji mwingine yoyote.
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Ureno, amesema pamoja na
kutofurahia maamuzi ya Hazard kumpa ruhusa Drogba kupiga penati ya
kwanza katika mchezo huo, bado alijihisi kawaida kutokana na mkwaju wa
mshambuliaji huyo kutoka nchini Ivory Coast kutinga nyavuni na
kuizawadia bao la pili Chelsea.
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni