KARIBU

Jumanne, 28 Oktoba 2014

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale ndio mchezaji wa kipekee wa Uingereza kuorodheshwa kati wachezaji wanaoshindania tuzo la mchezaji bora zaidi duniani Ballon d’Or huku mshambulizi matata wa Real Madrid Christiano Ronaldo akitarajiwa kuhifadhi taji hilo

Bale, mwenye umri wa miaka 25, aliweza kuifungia Real Madrid mabao 22 msimu uliopita na kuwezesha Real Madrid kunyakua kombe la kilabu bingwa duniani
Lionel Messi ambaye ameshinda taji hilo mara tatu pia yuko miongoni mwa orodha hiyo akiwa na mwenzake Neymar
Orodha hiyo ya wachezaji 23 itapunguzwa hadi watatu ambapo mshindi atatangazwa mnamo Januari 12, 2015 huko mjini Zurich .
Hatahivyo hakuna nafasi ya mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez ambaye alikuwa kiungo muhimu katika kuisadia timu yake ya nyumbani Uruguay kufika katika robo fainali ya michuano ya kombe la dunia nchini Brazil,lakini akasimamishwa kwa mda kushiriki katika soka yoyote kwa miezi mine kwa kumng’ata mlinzi wa Italy Giorgio Chiellini.

Mapenzi Ni Kitu Ambacho Kina Nguvu Sana Katika Dunia Mwanamuziki Usher Raymond Ameamua Kuweka Siri Zote   Hadharani Licha Ya Kuwa MpenziWake Huyo Amemzidi Umri.



 Lakini Amemsifia Kwa Kusema Ni Mwanamke Mwenye Mapenzi Ya Kweli Pia Ni Mshauri Wake Mkubwa  Sababu Amechukuwa Nafasi Kubwa Katika Maisha Yake.

 Ni Mwanamke Mwenye Kujituma Na Mwenye Ubinadamu Pasipo Kujali Umaarufu Wa Usher  "nampenda Sifikirii Kuachana Nae  Ni Mwanamke Ambae Anajitambua".

 Mpenzi Wake Anaitwa Grace Miguel Na Ndio Meneja Wake Ambae Anasimamia Kazi Zake Zote Za Muziki Na Mambo Yake Mengine.

Jumatano, 22 Oktoba 2014

Rais wa Marekani, Barack Obama, ametoa kauli yake kuhusu mwanamume aliyeshikwa na wivu baada ya yeye kumbusu mpenzi wake kwenye mashavu.

"rais tafadhali usimguse mpenzi wangu," alisema mwanamume, aliyetambuliwa na CNN kama Mike Jones.
Yote hayo yalitokea wakati Obama alipokuwa anapiga kura ya mapema katika jimbo la Illinois karibu na mwanamke aliyetajwa tu kama Aia Cooper.
''Kusema kweli sikuwa nimepanga kufanya hivyo,'' alisema Rais Obama , huku akiendelea kupiga kura yake huku Copper akiangua kicheko.
Baadaye Copper aliyeonekana kushikwa na aibu aliomba radhi kwa niaba ya mpenzi wake.
Obama alionekana naye kashikwa na aibu na kusema kwa tabasamu kuwa ,''hiki ni kisa tu cha mwanamume ndugu yangu kutaka tu kuniabisha bila sababu,''
Baada ya maongezi ya muda mfupi kati ya Obama na Cooper, wawili hao walimaliza kupiga kura, na kamera ikaonyesha Obama akimbusu Cooper mashavuni na kumpa mpenzi wa Coopper sababu nyingine ya kuongea.

Kenya kushiriki kombe la walemavu

Kenya na Ghana ndiyo mataifa pekee kutoka Afrika yatakayoshiriki kwenye mashindano ya kombe la dunia ya kandanda ya walemavu nchini Mexico mwezi ujao.

Uzbekistan ndio bingwa mtetezi wa mashindano hayo yatakayojumuisha timu 24.
Hii ni mara ya kwanza Kenya kushiriki mashindano haya ya kombe la dunia kwa wachezaji wa kandanda ya walemavu. Kocha Morris Shikanda anasema matumaini yao ni haba.
''Haja yetu kubwa ni kupata ujuzi katika mashindano hayo, sisi hatuna ujuzi kama Ghana lakini ni jambo la maana sana kushiriki. Tunaomba serikali na wahifadhi wengine watusaidie,’’ asema Shikanda.
Nahodha wa timu ya Kenya Ibrahim Wafula anasema walifuzu kwa kombe la dunia wakati wa mashindano ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Liberia mwaka jana mwezi Disemba, na kwamba tofauti na timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars ambao walisafiri Brazil kutizama kombe la dunia wao watakua uwanjani.
''Sisi tutacheza, na tunajivunia hilo licha ya ulemavu wetu tumekua timu ya kwanza Afrika Mashariki kucheza kwenye kombe la dunia. Hatuendi Mexico kama watazamaji jinsi walivyofanya Harambee Stars,’’ asema Wafula.
Mwandishi wa michezo wa BBC John Nene anasema Liberia na Ghana ni miongoni mwa mataifa hodari barani Afrika kwenye kandanda ya walemavu.
Mmoja ya wachezaji wa Kenya Dedan Ireri, ambaye anafanya kazi ya uchuuzi, asema anafurahishwa na maendeleo ya mchezo huu Afrika licha ya matatizo yanayowakumba nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa jumla.
Liberia na Sierra Leone yamejiondoa kwa sababu ya ugonjwa wa Ebola nchini humo.


Mchezaji wa soka nchini India, Peter Biaksangzuala amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kuanguka vibaya uwanjani akisherehekea bao lake.

Mchezaji huyo alikuwa na umri wa miaka 23 na alijeruhi uti wake wa mgongo baada ya kupiga pindu uwanjani akisherehekea bao lake la kusawazisha kw atimu yake Bethlehem Vengthlang FC dhidi ya Chanmari West FC.
Biaksangzuala alikimbizwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji lakini baadaye alifariki.
Mechi hiyo ambapo alipata jerehe la mgongo, ilikuwa mechi muhimu katika ligi ya nchi hiyo.
Taarifa kutoka kwa ligi hiyo kpitia kwa mtandao wa Facebook, ilisema : ''imekuwa siku yenye huzuni mkubwa kwa ligi ya Mizoram na kifo cha mchezaji wetu kimetushtua sana pamoja na wachezaji wenzake, wachezaji wa soka na mashabiki wa Mizoram. ''
"Peter alikuwa mchezaji mzuri na milizni mzuri sana, na pia alikuwa mchapa kazi.''

Baada tu ya wiki mbili katika nyumba ya Big Brother Mwakilishi mmoja wa Kenya Sabina ametimuliwa.

Sabina ana mtoto wa miezi minane na ndio mkenya wa kwanza kutimuliwa kutoka katika nyumba hiyo.
Inadaiwa kuwa watazamaji na mashabiki wa makala hiyo waliamua kumuondoa Sabina baada ya siku 14 pekee ili aende kumuhudumia mwanawe.
Sabina alionekana kumkosa sana mwanawe na wakati mwingi alionekana akifunga vitu kwenye mgongo wake ungedhani anambeba mtoto.
Aliweka pamoja blanketi na nguo na kuvifunga kwenye mgo wake akiwa na kofia ya mwanawe huku akitembea katika nyumba hiyo kabla ya kujiunga na wenzake waliokuwa wakijivinjari nje.
Baadhi wanasema kufunga vitu mgongoni ndio chanzo za mashabiki kuanza kuomuonea huruma Sabina wakisema bora aende nyumbani kwa mwanawe mwenye miezi minane.
Na hapo ndipo walipompigia kura Jumapili na kumtimua kutoka katika Big Brother house.
Sabina alitimuliwa kutoka katika nyumba hiyo pamoja na Lilian kutoka Nigeria na Esther wa Uganda.
Hatua ya kumondoa Sabina katika Big Brother house inamwacha mwakili mmoj tu wa Kenya Melvin Alusa ambaye ni kakake Ben aime Baraza wa kikundi cha wanamuziki cha Sauti Sol.
KILICHOWASHANGAZA MASHABIKI BAADA YA  MOURINHO KUZUNGUMZIA PENATI ILIYOPIGWA NA DROGBA
Meneja wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amewashangaza waandishi wahabari baada ya kusema hakufurahishwa na kitendo cha kiungo mshambuliaji Eden Hazard kumuachia mshambuliaji Didier Drogba kupiga  penati ya kwanza iliyopatikana wakati wa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko jijini London nchini Uingereza.
Mourinho, amesema jukumu la kupiga penati katika kikosi chake lipo mikononi mwa Eden Hazard lakini cha kushangaza alimuona kiungo huyo kutoka nchini Ubelgiji akimpa ruhusa Drogba kutimiza jukumu ambalo halikumuhusu.
Mourinho, amesema hakufurahishwa na kitendo hicho na amewataka waandishi wa habari kutambua wazi kwamba chaguo lake katika jukumu la kupiga penati inapojitokeza katika michezo ya The Blues ni Hazard na si kwa mchezaji mwingine yoyote.
Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Ureno, amesema pamoja na kutofurahia maamuzi ya Hazard kumpa ruhusa Drogba kupiga penati ya kwanza katika mchezo huo, bado alijihisi kawaida kutokana na mkwaju wa mshambuliaji huyo kutoka nchini Ivory Coast kutinga nyavuni na kuizawadia bao la pili Chelsea.
.