Ligi Kuu Bara Kuendelea Mwishoni Mwa Juma
Ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2014-15 kesho
itaendelea tena kwa michezo ya mzunguuko wa pili kuchezwa katika viwanja
kadhaa ambapo kikosi cha Wekundu wa Msimbazi Simba kitakuwa katika
uwanja wa nyumbani jijini Dar es salaam kupambana na maafande wa jeshi
la polisi kutoka mkoani Morogoro.
Simba watashuka katika dimba la taifa hiyo kesho huku wakiwa na kumbu kumbu ya matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Costal Union, ili hali upande wa Polisi Morogoro watakuwa na dhana ya kutotaka kurejea makosa waliyofanya katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi Azam FC ambao walichomoza na ushindi wa mabao matatu kwa moja.
Kocha wa Polisi Morogoro Mohamed Adolf Richard amesema baada ya kukiandaa vyema kikosi chake, ana hakika mambo yatakuwa barabara katika mchezo huo wa kesho.
Mchezo mwingine hiyo kesho utashuhudia mabingwa watetezi Azam FC wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani Azam Complex dhidi ya maafande kutoka mkoani Pwani, Ruvu Shooting.
Huko Manungu Tuariani mkoani Morogoro Mtibwa Sukari watakuwa wenyeji wa kikosi cha Ndanda FC (Mtwara Kuchele) ambacho kinashiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa mara ya kwanza.
Michezo mingine ya ligi hiyo itachezwa siku ya jumapili.
Dar es salaam Young Africans Vs Tanzania Prisons (Taifa Stadium)
Mbeya City Vs Costal Union (Sokoine Stadium)
Mgambo JKT Vs Stand Utd (CCM Mkwakwani)
JKT Ruvu Vs Kagera Sukari (Azam Complex)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni