KARIBU

Jumamosi, 1 Novemba 2014


Blaise Compaore alijiuzulu baada ya kushuhudia maandamano yenye ghasia baada ya jitihada zake za kutaka kuliongoza taifa hilo kwa awamu nyengine kupitia bunge kugonga mwamba.

Akizungumza hapo jana kanali Zida amesema kuwa Jenerali Traore hawezi kuliongoza taifa hilo.
''Nimechukua jukumu la kuliongoza taifa hili na serikali ya mpito ili kuliendeleza na kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya kidemokrasia kwa njia ya amani'' alisema kanali Zida katika hotuba yake katika runinga.

Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa chanzo cha kuaminika zinaeleza kuwa muigizaji mkongwe Mzee Manento amefariki dunia.

Mzee Manento atakumbukwa hasa katika filamu alizocheza kiumakini na marehemu Kanumba. Hero of the church, Dar to Lagos,Fake Pastor n.k pumzika kwa Amani
Mungu ailaze Roho ya maerehemu mahali pema peponi amina.
Bado tutaendelea kukuhabarisha chanzo cha kifo cha marehemu Mzee Mnento endelea kusikiliza 100.5 Times FM kwa Taarifa na Burudani mbalimbali.

Waumini wa kanisa katoliki la St. Francis mjini Diani kusini mwa pwani ya Kenya walipigwa na butwaa baada ya baadhi yao kuzuiwa kuingia katika kanisa hilo kutokana na mavazi yao yaliokuwa nusu uchi.

Julia baraza ambaye alikuwa amevalia kisibao ,ukanda wa manjano na viatu vyenye kisigino kirefu alishangazwa na sheria hizo mpya ambazo zilimsababisha kukosa misa ya asaubuhi.
Kulingana na gazeti la the standard nchini kenya,Julia alisema kuwa watu wawili walimsimamisha nje ya mlango wa kanisa hilo na kumwambia kwamba mtindo wake wa mavazi ulipigwa marufuku katika kanisa hilo na kwamba ametakiwa kuvaa mavazi ya heshima.
Aidha wasichana waliokuwa wamevalia suruali walilazimishwa kujifunga leso juu yake.
Julia alisema kwamba iwapo makanisa yataanza kufuata sheria kama hizo basi wengi hawatahudhuria maombi.
Baadhi ya waumini wamesema kuwa mhubiri wa kanisa hilo aliyejulikana kama Joseph pekee alikuwa ametangaza katika ibada ya awali kwamba mavazi yasio ya heshima hayatakubalika katika kanisa hilo.

Kulala na wanawake wengi kunapunguza hatari ya kupatikana na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo,kulingana na utafiti.

Katika utafiti uliochapishwa katika jarida la saratani,Watafiti kutoka chuo kikuu cha Montreal wamebaini kwamba ikilinganishwa na wanaume walio na mpenzi mmoja katika maisha yao yote,kulala na zaidi ya wanawake 20 kunapunguza uwezekano wa kupatikana na ugonjwa huo kwa asilimia 28.
Wanaume 3,208 walishiriki katika utafiti huo ambapo kati yao Wanaume 1,590 walipatikana na ugonjwa huo kati ya Septemba mwaka 2005 na Agosti mwaka 2009.
Kwa jumla watafiti hao walibaini kwamba wanaume wenye saratani ya kibofu cha mkojo kuna uwezekano mara mbili kwa wao kuwa na watu wa familia zao wenye saratani.
Hatahivyo ushahidi unaonyesha kwamba idadi kubwa ya wapenzi wa kike miongoni mwa wanaume inapunguza tishio la ugonjwa huo.
Mwanamume anapojamiana na zaidi ya wanawake 20 katika maisha yake,tisho la kupata ugonjwa huo linapoungua kwa asilimia 28 mbali na asilimia 19 kwa aina yoyote ya ugonjwa wa saratani.
Utafiti huo pia umebaini kwamba mmoja kati ya wanaume wanne wa kiafrika hupatikana na saratani

Mume mgomvi aandaliwa mlo wa kondomu

Mwanamke mmoja mwenye watoto watatu katika wilaya ya Kole nchini Uganda alimuandalia mumewe mlo wa mipira ya kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha kati yao.

Mwanamke huyo ambaye ni mkaazi wa eneo la Arao aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina ya "Trust" kutoka duka jirani kabla ya kuzipika na kumuandalia mumewe kama chakula baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda, mwanamke huyo aliikata kata mipira hiyo ya kondomu ambayo ilikuwa haijatumika katika vipande vidogo vidogo na kuvichemsha kwa muda kabla ya kuvikaanga kwa mafuta ya kupikia na viungo vingine.
Wakati mumewe alipowasili kutoka kubugia pombe katika eneo jirani la kibiashara la Odede,aliandaliwa mlo huo katika sahani tofauti moja ikiwa na mipira hiyo kama mboga na nyingine ikiwa na mkaa.
Lakini jamaa huyo alibaini njama za mkewe baada ya kuonja mlo huo na kugundua ulikuwa na ladha tofauti.
Hatua hiyo ilikuwa ikilenga kumfunza mume huyo ambaye amedaiwa kuzua ugomvi na mkewe kila anapolewa na kurudi nyumbani.


 Muigizaji Wa Filamu Angelina Jolie Abadilisha Muonekano Wa Nywele Zake Kutoka Nyeusi Mpaka Kuwa Blonde A ngelina  Kaonekana Na Muonekano Huo Wakati Akimalizia Kufanya Filamu Yake Ndani Ya Maji Akiwa Na Mme Wake Brad Pitt.

Utafiti mpya umewaunga mkono wanawake wazee walio na wapenzi vijana.

Utafiti huo unasema kwamba wanawake wazee wanaotaka kupata watoto ni sharti watafute vijana wadogo.

Huku tafiti nyengine zikishindwa kubaini iwapo wanaume hufikia miaka ya kushindwa kuzaa,utafiti huu mpya kutoka Chuo kikuu cha Mc Gill nchini Canada umegundua kwamba ni vigumu kwa wanawake wazee kupata watoto na wanaume wa rika lao.
Utafiti huo unasema kuwa ijapokuwa wanaume hawana kiwango cha mwisho cha kutafuta watoto,fursa hiyo hupotea kila miaka inavyozidi.
Wakati unapotafuta watoto basi umri wa mwanamume ni muhimu tu kama ule wa mwanamke.
Utafiti huo uliwahoji takriban wanawake 631 walio na umri kati ya 40 na 46 pamoja na wapenzi wao walio na umri kati ya 25 na 70.
Wanawake hao baadaye waligawanywa katika makundi mawili kulingana na iwapo ni wazazi au la.
Watafiti hao wamebaini kwamba wanaume walio na miaka 43 na kuendelea uwezo wao wa kupata watoto uko chini ikilinganishwa na wale wa chini ya umri huo.
Utafiti huo pia umebaini kwamba wanawake wengi huanza kukosa kushika mimba wakiwa na miaka 40 huku wanaume nao wakianza kubahatisha wafikapo miaka 43.